![]() ![]() ![]() Shahada ya Uzamifu katika Idara hii hutolewa kupitia kwa uandishi wa tasnifu. ![]() Sasa hivi Idara ina zaidi ya wanafunzi 200 wa Shahada ya Uzamili. Masomo ya Shahada ya Uzamili ya Kiswahili hudumu miaka miwili: ikiwa ni mihula mitatu ya kazi za darasani na muhula mmoja wa kuandika tasnifu au mihula miwili ya kazi za darasani na mihula miwili ya kuandika tasnifu. Wanafunzi hawa hutathminiwa kupitia kwa kazi ya darasani na mitihani. Idara hii hufundisha wanafunzi wa shahada za B.A. Idara hii inatambulika kwa ukubwa wake tukizingatia idadi ya wanafunzi na ubora wa kozi zinazofundishwa. Wahadhiri hawa wana ujuzi wa miaka mingi katika maeneo ya utaalamu kama vile: Idara hii inao wahadhiri kumi na tisa (19) katika mabewa tofauti ya chuo hiki (Bewa Kuu, Mombasa na Nakuru). Idara hii ipo kwenye Barabara ya Makongamano (Conference Road), karibu na Idara ya Fasihi, Lugha na Isimu, ikiwa nyuma ya Kituo cha Biashara na mkabala na kanisa dogo la chuo kikuu. Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika ilianzishwa mwaka 1987 wakati Idara ya Isimu na Lugha za Kiafrika ilipogawanywa kuwa Idara tatu ambazo ni: Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Idara ya Lugha za Kigeni na Idara ya Kiingereza. ![]()
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorWrite something about yourself. No need to be fancy, just an overview. ArchivesCategories |